FAQs

wananchi wanaouzunguka mradi watafaidika kwa kupata ajira za muda mfupi na na ajira za muda mrefu katika hatua zote za mradi kuanzia utafiti hadi uzalishaji. Hali ya uchumi ya wananchi itakuwa bora kutokana na kujihusisha na miradi ya matumizi ya moja kwa moja kama kilimo cha maua na mboga mboga, ufugaji wa samaki na kadhalika. Vilevile, maeneo ambayo miradi itatekelezwa wananchi watapata fursa za kibiashara kama biashara ya chakula na huduma za malazi.

Ni vigumu kulinganisha unafuu wa nishati ya jotoardhi na nishati zingine, sababu kila nishati ina asili yake na hatua zake kabla ya kufika kwa mtumiaji.

Unafuu wake mkubwa wa nishati ya jotoardhi huonekana zaidi katika maeneo yafuatayo;-

i.Nishati ya jotoardhi haiathiriwi na hali ya hewa, uzalishaji wake ni endelevu hautegemei jua wala upepo. Mathalani, kiasi cha umeme kinachozalishwa mchana au usiku ni kilekile.

ii.Gharama kubwa ni katika hatua za mwanzo yaani utafiti na uchimbaji. Lakini uendeshwaji wake ni wa gharama nafuu sana.

iii.Uzalishaji wake ni rafiki kwa mazingira

Tafiti za nishati ya jotoardhi huchukua muda mrefu kabla ya kuanza kuvunwa. Mathalani, tafiti huchukua takribani miaka 7 kuanzia utafiti wake mpaka uzalishaji. Hivyo, kwa Tanzania hatua tuliyofikia kama shughuli zitaenda kwa mtiririko ulivyo pangwa mwaka 2022 uzalishaji unatarajiwa kuanza.

Tangu kuanzishwa kwa TGDC mwaka 2014 imeendelea kujengea uwezo wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi, mafunzo hayo yamendelea awamu kwa awamu. Sanjari na mafunzo hayo kunajitihada zimeendelea kufanywa na TGDC kwa ushirikiano na taasisi za elimu ya juu nchini ili kuhamasisha wanafunzi kuingia katika tasnia ya nishati jotoardhi.

Kampuni inatilia mkazo sana suala la ushirikishwaji wa jamii hususan katika maeneo yanayo zunguka miradi ya jotoardhi. Jamii hushirikishwa kabla ya kuanza kwa tafiti na wakati wa tafiti zinaendelea jamii hufahamishwa kila hatua. Ushirikishwa huu hufanyika kwa mikutano kuanzia ngazi ya vijiji, kata, wilaya na mkoa.


Nishati ya jotoardhi inamanufaa yafuatayo;-

i.Ni nishati asilia na jadidifu.

ii.Inapatikana kwa uhakika mkubwa zaidi.

iii.Uzalishaji umeme wa uhakika (base load generation).

iv.Hupunguza athari mbaya za mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.

v.Hutoa nishati safi na salama kwa kutumia ardhi kidogo.

vi.Teknolojia iliyothibitishwa kisayansi na inazidi kuimarika.

vii.Inaweza kuongezwa/kupanuliwa ili kukidhi mahitaji kwa kutumia eneo dogo.

Hutumika kuzalisha umeme na matumizi ya joto ya moja kwa moja (Direct uses)

ix.Hupunguza moshi wa hewa zinazochafua mazingira.


Matumizi ya moja kwa moja ya nishati ya jotoardhi ni pamoja na;

Kupasha moto mitambo viwandani

Kupasha joto nyumba vitalu (green house) kwa ajili ya kilimo

Kupoza na kugandisha

Kukaushia mazao ya kilimo

Kupasha joto maji kwenye mabwawa ya kufugia samaki na ya kuogelea

Shughuli za utalii

Hutumika kwa tiba

Nishati ya jotoardhi (mvuke) ikiwa katika nyuzi joto 107 hasi nyuzi joto 300 hutumika kuzalisha umeme kwa kutumia Nishati mitambo (mechanical energy) katika ‘Turbine’ na nishati mitambo hubadilishwa kuwa nishati umeme katika genereta (Generator). Hivyo kupata umeme unaosafirishwa katika miundombinu ya usafirishaji kwa ajili ya teknolojia mbalimbali. Mitambo maalumu ya kufua umeme (Turbine) huzungushwa na mvuke unaotoka ardhini katika mkandamizo mkubwa. Nishati mkandamizo (Pressure energy) inayotoka sambamba na mvuke chini ya ardhi hubadilishwa na kuwa matumizi.