News

Posted date: 20-Sep-2022

ZIARA YA BODI YA WAKURUGENZI YA TGDC KATIKA KUTEMBELEA MIRADI YA JOTOARDHI YA KIEJO-MBAKA (MW 10), NGOZI (MW 30) NA SONGWE (MW 5)

News Images

Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme wa Jotoardhi usiopungua MW 5000 zinazopatikana katika maeneo zaidi ya 50 katika mikoa 16 nchini. Lengo la Kampuni la muda mfupi ni kuzalisha MW 200 za umeme zitokanazo na Jotoardhi ifikapo mwaka 2025 na megawati 500 za joto zitokanazo na nishati ya Jotoardhi. Ili kufikia lengo la kuzalisha MW 200 za umeme, TGDC inatekeleza miradi 5 ya kipaumbele ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradi hiyo ni Ngozi (MW 70) na Kiejo-Mbaka (MW 60) iliyopo Mbeya, Songwe (MW 5) - Mkoani Songwe, Luhoi (MW 5) - Pwani, na Natron (MW 60) - Arusha.