News

Posted date: 19-Apr-2024

TGDC Kuchoronga Visima vya Jotoardhi-Ngozi, Mbeya

News Images

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga Wakaa kikao na Uongozi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika Ofisi ya Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Bungeni Dodoma na kujadili maendeleo na mustakabali wa uendelezaji wa miradi ya kipaumbele ya jotoardhi hasa mradi wa Ngozi wa Mkoani Mbeya uliopo katika hatua ya kuhakiki rasilimali ya jotoardhi, ambayo kwasasa kazi ya uchorongaji inategemewa kuanza.

Aidha katika kikao hicho Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ameiagiza TGDC kuhakikisha kuwa inaharakisha uchorongaji katika mradi wa Ngozi ili miradi huu wa jotoardhi uanze kuzalisha umeme wa Jotoardhi kama azma ya Serikali inavyotaka. Amesema kuwa sasa ni wakati wa kutoa matokeo ya jotoardhi ili umeme huu ambao ni jadidifu na endelevu unufaishe wananchi.

Katika kikao hicho, TGDC iliongozwa na Meneja Mkuu Mathew Mwangomba, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Shakiru Idrissa Kajugus na Mhadisi wa Utafiti Doreen Mlele. Kwa upande wa TGDC, Meneja Mkuu amepokea na kuahidi kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kutoa matokeo ili nishati ya jotoardhi iweze kutumika nchini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo dunia inaikumbuka kwa sasa.