News

Posted date: 26-May-2025

PM Hon. Majaliwa Witnessed MoU Signing between Tanzania and Japan, TGDC included

News Images


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano ya ushirikiano wa Sekta mbalimbali kati ya nchi ya Japan na Tanzania ikiwemo Sekta ya Nishati.

Kwa upande wa Sekta ya Nishati taasisi inayosimamia uendelezaji wa Jotoardhi (TGDC) imetiliana saini makubaliano na kampuni ya Toshiba energies solutions huku Serikali kwa niaba ya TPDC iikiwekeana makubaliano na kampuni ya JCG leo 26 Mei, 2025 ya nchini Japan ambapo watashirikiana kwenye eneo la Jotoardhi na kujenga uwezo wa Teknolojia ya kusindika gesi (liquified Natural gas).

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa nchini Japan ambapo Wizara ya Nishati iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt Khatibu Kazungu.

Mhe Majaliwa amezishukuru kampuni za Japan kwa kuingia makubaliano hayo katika kipindi hiki cha Maonesho ya Biashara ya Dunia ya Osaka Expo ambayo hufanyika kila baada ya miaka mitano.

Waziri Mkuu ameahidi kuendelea kushirikiana na Japan kwenye uendelezaji wa sekta mbalimbali.

Makubaliano yaliyotiwa saini yanahusisha pia kuwajengea uwezo watanzania juu ya kutekeleza miradi ya kusindika gesi asilia, kutangaza fursa za uwekezaji kati ya TIC na Excel Africa pamoja na ZIPA.

Makubaliano mengine ni kati ya Kampuni ya Jotoardhi na Toshiba, Chuo Kikuu cha Dodoma na kampuni ya Japan, pamoja na makubaliano kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na taasisi ya hospitali ya Tokushukai.

Aidha, kupitia makubaliano hayo, kampuni ya Jotoardhi itaweza kunadi uwepo wa rasilimali zake kiasi cha megawati 5000 ambazo zinapatikana kwenye mikoa 16 huku ikiwa na maeneo ya zaidi ya 52 yenye viashiria vya jotoardhi.