Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Memba wa Bodi

Mr. Beatus Peter Segeja (Chairman)

Mkurugenzi wa Utawala na Huduma benki ya CRDB Bank PLC. Alijiunga na Bodi tarehe 19 Agosti 1982. Kabla ya cheo cha sasa alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Meneja wa Uthibitishaji Malipo na Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi katika Benki ya CRDB. Ana CPA(T). Ana Diploma ya Juu ya Uhasibu kutoka Nyegezi Social Institute of Accountancy.


Eng. Felchesmi J. Mramba

Mkurugenzi asiye Mtendaji, alihitimu shahada ya kwanza ya Sayansi ya Uhandisi Umeme kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara na ni mwanachama wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB). Mhandisi Mramba hivi sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Umeme Tanzania, TANESCO, na ana uzoefu mkubwa katika sekta ya umeme. Ana weledi wa kutosha katika utawala wa biashara, ubunifu miradi, ununuzi wa umma, usomamizi wa rasilimali na uendelezaji wa nishati.