Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

TAARIFA KWA UMMA: MRADI WA NGOZI WA KUVUNA NISHATI YA JOTOARDHI KWA AJILI YA KUCHORONGA VISIMA VYA AWALI Imewekwa: 17th February, 2017

Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) ilianzishwa Disemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongoza maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania. TGDC ni kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalomilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa 100%. Kampuni ilianza rasmi shughuli zake Julai, 2014 kwa jukumu na mamlaka ya kutafiti, kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi kwa uzalishaji umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.

TGDC inatarajia kuchoronga visima vya awali ikiwa ni hatua ya mwanzo katika kuvuna nishati ya jotoardhi. Hivyo uchambuzi wa athari za mazingira na jamii (ESIA) utafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 (Environmental Management Act Cap 191 of 2004) na kanuni zake za mwaka 2005 (Environmental Impact Assessment and Audit Regulations of 2005), lengo ni kuainisha faida lakini pia athari za mradi kabla ya utekelezaji.

Wataalam wa jamii na mazingira wanatarajia kufanya mikutano na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya mradi kuanzia tarehe 6 hadi 12 Machi, 2017 katika wilaya za Rungwe (Goye tarehe 6 Machi na Ishinga ni 7 Machi) na Mbeya vijijini (Nsongwi Juu tarehe 8 Machi, Hapyo ni 9 Machi na Nsenga ni 10 Machi, 2017).

Kwa taarifa hii tunaomba wadau wote na wananchi kwa ujumla wenye maoni ushauri na mapendekezo juu ya mradi huu kutuma maoni yao kupitia anuani iliyopo hapo chini katika kipindi cha wiki mbili (2) tangu kutolewa kwa tangazo hili.

Anuani: Meneja Mkuu, Ofisi ya TGDC, S.L.P 14801, Dar es salaam, Ofisi ya TANESCO Mkoa wa Mbeya au Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Rungwe.

Imetolewa na: Ofisi ya Mawasiliano

Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania-TGDC

Dar-es-salaam

Barua pepe: communication.tgdc@tanesco.co.tz